Mtuhumiwa mmoja ameuawa na mwingine ameripotiwa kuwa yuko mahututi . Uchunguzi wa polisi kuhusu mkasa huo unaendelea huku polisi wakisema wameikuta silaha inayoweza kusababisha mlipuko kwenye gari linalohusishwa na mmoja wa watuhumiwa wa mauaji hayo.
Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema mauaji hayo yaliwalenga Wayahudi wa Australia mamlaka zinafanya kazi kuchunguza waliohusika na kuyafanya mauaji hayo.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiwemo Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa bunge la Ulaya Roberta Metsola na Mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Kaja Kallas wamelilaani vikali tukio hilo. Ufaransa, Israel, Ujerumani, Uhispania ni miongoni mwa mataifa yaliyolaani pia vikali shambulio hilo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii