Mafuriko ya ghafla yauwa watu 21 Moroko

Mafuriko ya makubwa yaliyotokana na mvua kubwa na ya ghafla yameuawa watu 21 katika mji wa pwani ya Moroko wa Safi.

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha maji yaliyochanganyika na matope yakizikokozowa gari na takataka kwenye mitaa ya mji huo ulio umbali wa kilomita 300 kusini mwa mji mkuu, Rabat.

Mamlaka zinasema nyumba zipatazo 70 kwenye mji huo wa kihistoria zimeharibiwa vibaya. Watu wengine 32 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kuwasaka manusura, huku mamlaka za utabiri wa hali hewa zikitangaza kwamba mvua kubwa zaidi inatazamiwa kesho Jumanne.

Kwa mwaka wa saba mfululizo, taifa hilola kaskazini mwa Afrika limekuwa likikabiliwa na ukame, mafuriko na hali mbaya ya hewa mara kwa mara.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii