Magari 11 yaondolewa namba za usajili Rukwa

Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Rukwa limefanya operesheni maalum ya usalama barabarani kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, ikilenga kulinda usalama wa wasafiri na watumiaji wa barabara.

Katika operesheni hiyo, magari 37 ya abiria yalikaguliwa na 11 kubainika kuwa na hitilafu za kiufundi, hivyo kuondolewa barabarani hadi yatakapokidhi vigezo vya usalama.

Polisi wamewaonya madereva dhidi ya mwendo kasi, ulevi, kuzidisha abiria na makosa mengine ya barabarani.

Aidha, Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Rukwa Mrakibu wa Polisi Chabruma Gama, ametoa onyo kali kwa madereva, makondakta na maajenti wa mabasi dhidi ya kupandisha nauli kiholela, wakisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka taratibu, huku Abiria wakipongeza juhudi hizo na kuahidi kutoa ushirikiano.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii