Rais wa Marekani Donald Trump amelihutubia taifa hilo leo Alhamisi ya Disemba 18 mwaka huu na kuweka wazi mipango yake ya kuifanya Marekani kuwa imara zaidi kuliko hapo awali.
Rais Trump alianza hotuba yake kwa kutaja orodha ndefu ya kile anachokiona kama mafanikio yake katika mwaka wake wa kwanza akiwa madarakani.
Aidha alisema kuwa licha ya kuirithi nchi ikiwa katika hali mbaya kutoka kwa mtangulizi wake Joe Biden lakini wamefanikiwa kuleta mabadiliko chanya kuliko rais mwingine yoyote katika historia ya Marekani ambapo miongoni mwa masuala aliyoyagusia kwa kifupi ni uhalifu, uhamiaji vita dhidi ya dawa za kulevya na kuliimarisha tena jeshi la Marekani.
Hata hivyo amegusia pia suala la kupunguza bei ambalo linaibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa Wamarekani na kuahidi taifa hilo kuimarika kiuchumi mwaka ujao katika kiwango ambacho ulimwengu haujawahi kushuhudia.