Bunge la Ujerumani lapitisha mabilioni ya matumizi ya jeshi

Kamati ya Bajeti ya Bunge la Ujerumani imeidhinisha kitita cha yuro bilioni 52 za matumizi ya kijeshi wakati taifa hilo likijaribu kujiimarisha katikati ya kitisho cha kiusalama kinachosababishwa na uchokozi wa Urusi.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Berlin Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius alisema kuwa uamuzi wa kuidhinisha matumizi hayo unaweka serikali na bunge katika mstari wa kutimiza ahadi za ulinzi.

Aidha vifaa vya kijeshi vitakavyonunuliwa ni pamoja na nguo, vifaa vya kujilinda kwa ajili ya wanajeshi vyenye thamani ya yuro bilioni 21 na magari 200 ya kivita ya Puma yenye thamani ya yuro bilioni 4.

Kamati hiyo ya bajeti ya bungeni ambayo husimamia manunuzi yote makubwa ya silaha ina mamlaka ya kupitisha bajeti hiyo bila ya idhini ya bunge zima.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii