Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada 200 wametahadharisha kwamba operesheni za kiutu kwenye maeneo ya Kipalestina na hasa Ukanda wa Gaza ziko hatarini kufungwa hayo yamesemwa kwenye taarifa yao ya pamoja kwamba shughuli hizo huenda zikafungwa ikiwa Israel haitaondoa vizuizi ambavyo ni pamoja na mchakato mgumu wa usajili.
Taarifa hiyo imesema kuwa hatua ya kufutwa kwa usajili wa mashirika ya misaada ya kimataifa huko Gaza itakuwa na athari kubwa katika upatikanaji wa huduma muhimu na za msingi.
Hata hivyo mashirika mengi ya misaada ya kimataifa huenda yakafutiwa usajili hadi kufikia Disemba 31 waka hii ikimaanisha kwamba yanapaswa kufunga shughuli zao ndani ya siku 60 ambapo Mashirika hayo yanasaidia huduma za tiba, makazi ya dharura, huduma za maji na usafi wa mazingira pamoja na vituo vya lishe kwa watoto wenye utapiamlo mkali.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime