Nigeria yaomba radhi Burkina Faso baada ya ukiukaji wa anga

Nigeria imeomba radhi Burkina Faso kufuatia ukiukaji wa anga yake wiki iliyopita. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria amepokelewa Jumatano, Desemba 17, na Kapteni Ibrahim Traoré huko Ouagadougou.

Yusuf Maitama Tuggara amesema kwamba alikuwa amebeba ujumbe wa "mshikamano na udugu" kutoka kwa Rais Ahmed Bola Tinubu kwa mwenzake wa Burkina Faso. Ujumbe wa Nigeria pia umejadili masuala yanayohusu kutua kinyume cha sheria kwa ndege ya Nigeria nchini Burkina Faso wiki iliyopita.

Nchini Burkina Faso, ujumbe wa watu watano, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na afisa wa kijeshi wa Nigeria, ulipokelewa katika ikulu ya rais huko Ouagadougou mnamo Desemba 17, mbele ya Kapteni Ibrahim TraorĂ© na Waziri wake wa Ulinzi. Majadiliano yalilenga hasa "kutua kwa dharura" kwa ndege ya kijeshi ya Nigeria huko Bobo Dioulasso.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Maitama Tuggar aliomba radhi kwa niaba ya nchi yake: "Inasikitisha kuona kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika hati hizo. Hii ni bahati mbaya, na tunaomba radhi kwa tukio hili baya."

Wiki iliyopita, ndege ya kijeshi ya C-130 ya Nigeria ililazimika kutua kwa dharura huko Bobo-Dioulasso, Burkina Faso, ingawa haikuwa na idhini ya kuruka juu ya anga ya Burkina Faso. Wafanyakazi 11 walikamatwa. Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, bado wako Burkina Faso na wanahudumiwa vizuri.

Hata hivyo, waziri hakutoa maelezo yoyote kuhusu uwezekano wa kuachiliwa kwao au kurejeshwa kwa ndege hiyo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii