Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto kwa magari mawili katika Kijiji cha Lusanga Wilaya ya Mvomero tukio lililotokea kufuatia kifo cha mfanyakazi wa ndani Mwanahasan Juma Hamis (18).
Katika uchunguzi wa kina wa jeshi la Polisi mkoani humo Mkama tukio hilo limetokea Desemba 17 mwaka huu wakati mwili wa marehemu ukisafirishwa kuelekea eneo la mazishi hivyo taarifa zinaeleza kuwa mvutano uliibuka baada ya ndugu wa marehemu kudai kuwepo kwa sintofahamu kuhusu hali ya mwili wake madai ambayo yalisababisha hasira miongoni mwa wananchi na kupelekea kuchomwa kwa magari hayo mawili.
Hata hivyo upande mwingine wa taarifa unaeleza kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umefanyiwa taratibu za kitabibu ikiwemo uchunguzi wa kitabibu jambo ambalo Polisi wamesema linaendelea kufanyiwa uchunguzi ili kubaini ukweli wa madai hayo.
Aidha Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake washirikiane na vyombo vya dola huku likiahidi kutoa taarifa kamili mara baada ya uchunguzi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime