Polisi Morogoro wachunguza kifo dada wa kazi, magari kuchomwa moto Mvomero

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto kwa magari mawili katika Kijiji cha Lusanga, Wilaya ya Mvomero, lililotokea kufuatia kifo cha mfanyakazi wa ndani, Mwanahasan Juma Hamis (18).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, tukio hilo limetokea Desemba 17, 2025, wakati mwili wa marehemu ukisafirishwa kuelekea eneo la mazishi.

Taarifa zinaeleza kuwa mvutano uliibuka baada ya ndugu wa marehemu kudai kuwepo kwa sintofahamu kuhusu hali ya mwili wake, madai ambayo yalisababisha hasira miongoni mwa wananchi na kupelekea kuchomwa kwa magari hayo mawili.

Hata hivyo, upande mwingine wa taarifa unaeleza kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umefanyiwa taratibu za kitabibu, ikiwemo uchunguzi wa kitabibu, jambo ambalo Polisi wamesema linaendelea kufanyiwa uchunguzi ili kubaini ukweli wa madai hayo.

Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu, kuacha kuchukua sheria mkononi na kushirikiana na vyombo vya dola, huku likiahidi kutoa taarifa kamili mara baada ya uchunguzi kukamilika.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii