Familia Yapata Pigo Baada ya Binti yao Aliyetoweka Kupatikana Amekufa Kikatili

Familia moja huko Embakasi, kaunti ya Nairobi, imeomboleza kufuatia kifo cha kutisha cha binti yao wa miaka 12, Patience Mumbe. 

Inasemekana mwanafunzi huyo wa darasa la saba alitoweka alipokuwa akicheza nje ya nyumba yake na ndugu zake na marafiki zake siku ya Alhamisi, Desemba 4.

Wazazi wake walianzisha msako mkali, wakitarajia kumpata akiwa hai, lakini wakapata taarifa za kifo chake siku mbili baadaye kupitia chapisho la Facebook.

Mwili wa Patience Mumbe ulipatikana wapi? Mwili wa Mumbe ulipatikana katika eneo la KAA Estate, Embakasi, huku dalili wazi kwamba alikuwa amekufa kikatili.

Wapelelezi waliochunguza eneo hilo walibaini kuwa msichana huyo mdogo alikuwa amefungwa mikono yake nyuma ya mgongo wake, kamba nyeusi ya viatu ikiwa imezungushwa mwilini mwake, na alikuwa akivuja damu usoni na sehemu yake ya siri.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii