Wahamiaji haramu 23 wakamatwa Geita

‎‎Idara ya uhamiaji  Mkoa wa Geita imeendelea na jitihada zake za kupambana na wahamiaji haramu kupitia misako na doria mbali mbali inayoendelea kufanyika Mkoani humo.

‎Oktoba 22 mwaka huu jumla ya wahamiaji haramu 23 wamekamatwa katika maeneo ya lukirini, Igate na  kasota katika wilaya Geita ikiwa ni muendelezo wa doria zinazofanyika kila siku ili kupambana na wahamiaji hao haramu.

Kwa upande wake ‎‎Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Geita Mrakibu Mwandamizi  wa Uhamiaji SSI Donald Lyimo amesema Ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Geita pamoja na wilaya zake bado inaendelea kufanya misako,kaguzi na chunguzi mbalimbali Ili kukabiliana na wimbi la wahamiaji  haramu hapa nchini.

‎‎Aidha SSI Lyimo amebainisha Kuwa Wahamiaji haramu wote waliokamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za uhamiaji sanjari na kusisitiza kuwa zoezi hilo ni la kudumu na kuwaasa wananchi wa Mkoa wa Geita waendelee kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo yao kuliko kuishi nao kinyemela.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii