Mahakama ya Wilaya ya Kasulu imewahukumu washitakiwa wawili Alphonce Gwalide ( 45) mkulima na mkazi Mvinza wilayani Kasulu na Jastine Yoramu (36) Mkulima na mkazi wa Mvinza wilayani humo kifungo cha kwenda jela miaka 20 baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kupatikana na silaha moja aina Gobore.
Washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Disemba 27,2024 huko Kijiji cha Mvinza wilayani Kasulu na kufikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 13 mwaka huu.
Akitoa hukumu hiyo Oktoba 21 mwaka huu Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Sara Mcharo amesema kuwa Mahaka imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hatimaye kuwatia hatiani washitakiwa kwa kosa hilo.
Hata hivyo Washitakiwa hao wamehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya kumiliki wa silaha kinyume cha sheria, ujangiri na uwindaji haramu, vitendo vinavyoharibu rasilimali za Taifa ikiwemo Wanyama pori.