Mahakama yaweka pingamizi la kukataa ushahidi wa video

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam imekubaliana na pingamizi la tatu lililowasilishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu na kukataa kupokea flashi na memori kadi kama ushahidi kutokana na shahidi huyo kutokakuwa na sifa ya kuwasilisha ushahidi huo Mahakamani kwa kuwa yeye ni mtaalamu wa picha mnato na sio mjongeo na aliyepaswa kuwasilisha ushahidi huo kwa mujibu wa sheria ni mtaalamu wa kisayansi wa makosa ya mtandaoni.

Mahakama imeamua kuwa shahidi wa tatu wa upande wa Mashtaka, Inspekta wa Polisi Samwel Kaaya (39) si mtaalamu wa uchambuzi wa video bali ni mtaalamu wa upigaji picha za kawaida ambazo ni mnato.

Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 22 mwaka huu na Jaji Dustan Nduguru kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo.

Lissu aliwasilisha hoja nne kupinga upokelewaji wa vielelezo hivyo akidai kuwa shahidi huyo hana sifa stahiki za kuwasilisha ushahidi huo Mahakamani.

Kwa sasa Mahakama ipo mapumziko ya saa moja baada ya mtuhumiwa Tundu Lissu kupinga shahidi huyo wa tatu ombi lake la kutaka taarifa yake ya uchunguzi ipokelewa na Mahakama badala ya hati aliyopaswa kuwasilishwa kwa mujibu wa sheria hoja ambayo imeleta mvutano na upande wa Jamhuri kuomba kupatiwa muda wa saa moja ili kupitia vifungu vya sheria.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii