Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Jubilate Lawuo amewahakikishia wananchi kuwa hali ya ulinzi na usalama kuelekea Oktoba 29 ni shwari kabisa.
Akizungumza na waandishi wa habari DC amesema kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo tayari kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, utulivu na kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za uchaguzi.
Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi bila hofu yoyote, akisisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anatumia haki yake ya kikatiba katika mazingira salama.
Pia aliwaonya watu wachache wenye nia ya kuvuruga mchakato huo kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akitoa rai ya kudumisha mshikamano na utulivu kwa manufaa ya taifa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi bila hofu yoyote, akisisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anatumia haki yake ya kikatiba katika mazingira salama.