Serikali kuongeza fursa za elimu kwa wenye mahitaji maalum

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maalum Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Magreth Matonya amesema Serikali inaendesha programu mbalimbali za elimu, ikiwemo ya kubaini wanafunzi wenye mahitaji maalum kuanzia ngazi ya kijiji kwa ajili ya maandalizi ya kujiunga na shule.

Akizungumza Oktoba 22 mwaka huu jijini Dodoma katika Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25, Dkt. Matonya amesema zoezi hilo linasimamiwa na Maafisa Elimu Maalum wa mikoa kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali.

Ameeleza kuwa Serikali pia inatekeleza Mwongozo wa Shule ya Nyumbani, ambapo walimu huwafikia wanafunzi nyumbani kila Ijumaa kwa ajili ya kujifunza kutoa ushauri wa kitaalam na kufanya mazoezi ya kielimu.

Aidha amesema kuna ongezeko kubwa la mwamko wa wazazi kuhusu elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum ambapo tangu mwaka 2020 idadi ya wanafunzi hao imeongezeka kwa zaidi ya mara tatu ikionyesha mabadiliko chanya katika mtazamo wa jamii kuhusu elimu jumuishi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii