David Kafulila ambaye ni Mkurugenzi wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri DART, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, ameandika.
Uamuzi wa serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopata mikopo kutoka 142,000 mwaka 2021 hadi 248,000 mwaka 2024 umefanyika kwa lengo la kusaidia watoto wanaotoka katika familia masikini ambao wanategemea mikopo ya elimu ya juu kumudu gharama za masomo.
Vilevile, hatua ya kuongeza posho ya kujikimu kwa wanafunzi wanaopata mikopo kutoka Shilingi 8,500 hadi Shilingi 10,000 kwa siku, baada ya kudumu kwa kiwango cha zamani kwa miaka mingi, imelenga kuwawezesha wanafunzi hao kukabiliana na gharama za maisha wakiwa chuoni.
Aidha, uamuzi wa serikali kupanua wigo wa mikopo hadi kuwahusisha wanafunzi wa ngazi ya Diploma ni hatua ya kihistoria ambayo imewanufaisha vijana wengi wanaotoka katika familia zenye kipato cha chini nchini.