Mnamo Oktoba 22 mwaka huu wajumbe kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) walishiriki kikao cha kimkakati kilichofanyika katika ofisi kuu za EACLC, eneo la Ubungo Terminal, jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kililenga kujadili uwezekano wa ushirikiano kati ya EACLC na China Shandong Tongshan Children Welfare and Public Welfare Development Centre, kikiongozwa na Mwenyekiti LI XIAO.
Mradi huu unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2026 ambapo Majadiliano hayo yalijikita katika pendekezo la kuanzisha mradi wa hisani unaolenga watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 12, kwa madhumuni ya kukuza ubunifu na vipaji katika sanaa za uchoraji na uchoraji rangi kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Kupitia mradi huo taasisi kutoka China imepanga kutoa vifaa vya kuchorea na kupaka rangi kwa wanafunzi watakaoteuliwa huku kipaumbele kikitolewa kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo wa wastani ili kuhakikisha ushirikishwaji kwa wote.
Taasisi hiyo ya China pia ilishiriki uzoefu wake wa mafanikio katika kutekeleza miradi kama hiyo nchini Uganda, Kenya, na Angola, na kuonesha utayari wa kuendeleza mpango huo hapa Tanzania.