Thamini Uhai yaunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa vifaa vya afya

Wizara ya Afya imepokea vifaa vya Ofisi kutoka asasi ya kiraia iitwayo Thamini Uhai ambapo imekabidhi samani za ofisi zikiwemo meza 2, viti 9 na kabati 3 kama sehemu ya mchango wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya utoaji huduma nchini.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Huduma za Uuguzi na Ukunga, Bw. Paul Magesa Oktoba 27  mwaka huu amesema ushirikiano kati ya Serikali na wadau ni muhimu ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi.

Aidha Bw. Magesa amesema mchango huo kutoka Asasi ya Thamini Uhai ni kielelezo cha kuthamini uhai kwa vitendo, kwani unachangia kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya na hivyo kuongeza ufanisi na tija kwenye utoaji wa huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai Bw. Banzi Msumi amesema vifaa hivyo ni sehemu ya juhudi za shirika hilo kusaidia Serikali kuboresha huduma za afya huku akisisitiza kuwa kama wadau wa sekta hiyo wana wajibu wa kushirikiana na serikali kuhakikisha huduma bora zinaendelea kutolewa kwa wananchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii