Hakuna habari yenye Thamani zaidi kuliko uhai wa mwandishi wa habari

              Usalama kwanza:

Katika ulimwengu wa uandishi wa habari tamaa ya kupata habari kubwa na ya pekee mara nyingine hupelekea waandishi kuhatarisha maisha yao.

Hata hivyo shirikisho la kimataifa la waandishi wa habari (IFJ) linasisitiza kwa nguvu zote kwamba hakuna habari yoyote inayostahili uhai wa mwandishi wa habari.

Kauli hii inapaswa kuwa mwongozo wa msingi kwa kila mhusika katika vyombo vya habari,kuanzia kwa wahariri,kwenye klabu zetu,kwa waandishi chipukizi wanaotafuta "habari kubwa" ya kuwainua kitaaluma.

Waandishi wa habari wanapaswa kujifunza kuishi na kufanyakazi kwa tahadhari ,ili kuepuka hatari kama vile majeraha kifungo,kufukuzwa,au vitisho vingine vinavyoweza kujitokeza katika mazingira ya kazi.

Hivyo basi,IFJ imeweka kanuni ya muhimu za kufuatwa kwa ajili ya usalaama wa waandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mambo ya kuzingatia kwa usaalama wa waandishi wa habari hususani katika kuelekea katika uchaguzi mkuu wa serikali Oktoba mwaka huu ni pamoja na:

1: Hakuna habari yenye thamani kuliko uhai wako: Jilinde.

Daima weka usalama wako mbele ya kila jambo. Habari nyingine zitaendelea kuwepo lakini maisha .hayana mbadala.

2: Zingatia maadili ya kitaaluma: Uandishi wa habari unahitaji uadilifu ,ukweli na uwajibikaji kwa umma.

3; Shughulikia habari za uchaguzi kwa usahihi na bila upendeleo. Habari za kisiasa zinahitaji umakini mkubwa ili kuepuka kuchochea migogoro au upotoshaji.

4:Usitumike na wanasiasa kutimiza malengo yao ya kisiasa. Kazi ya mwandishi ni kuripoti ukweli,si kuwa msemaji wa chama au mgombea.

5: Usitoe matamko ya wazi kwa niaba ya vyama vya siasa. Kufanya hivyo ni kuhatarisha heshima na uaminifu wa taaluma yako .

6: Usikubali nafasi za kisiasa,baki mwandishi wa habari .

 Kuchanganya uandishi wa habari na siasa ni kuvuruga mipaka ya maadili ya kazi.

7: Epuka sifa na kujisifu kupita kiasi. Sifa nyingi zinawez kupoteza umakini wa kazi na kuathiri maamuzi ya kitaaluma.

8: Epuka mgogoro wa maslahi. Usihusishe kazi yako ya uandishi wa habari na maslahi binafsi au biashara.

9: Usivae alama au mavazi ya vyama vya siasa kama vile kofia,fulana,au sare, mavazi kama haya yanaweza kuashiria upendeleo wa kuhatarisha usalaama wako.

10: Usijuhusishe katika mijadala ya hadhara kuhusu ubora wa chama au mgombea.

Mjadala wa aina hiyo unaweza kuharibu taswira yako ya kutokuwa na upendeleo.

11: Usikubali pesa wala rushwa . 

Rushwa huharibu uadilifu wa habari na kuua heshima ya taaluma ya uandishi.

12: Jua sheria za vyombo vya habari: Kutokujua sheria kunaweza kufanya utumie vibaya au kuingia matatani bila sababu.

13: Epuka siasa za kipuuzi au zisizo na tija. Kaa mbali na mijadala isiyo na misingi inayoweza kuhatarisha heshima yako.

14: Fuata miongozo ya usalama : Kumbuka kanuni za usalama wa kazi kila mara,hasa katika mazingira hatarishi.

15: Kuwa makini na vitisho,vyanzo vya habari vya uongo ,na uvamizi wa faragha.

 Jilinde dhidi ya hila ,vitisho au uandishi unaovuka mipaka ya haki za watu wengine. 

Uandishi wa habari ni taaluma yenye heshima kubwa lakini pia ni yenye hatari nyingi,ili kufanikiwa mwandishi wa habari anapaswa kuthamini maisha yake zaidi ya habari yoyote kuzingatia maadili ,nakufanya kazi kwa umakini na uadilifu.

Hivyo Uongozi wa chama chama cha waandishi wa habari mkoa wa kagera( KPC) unachukua fursa hii kutoa wito kwa waandishi wahabari mkoa wa kagera na Tanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa kufuata maadili ya taaluma zao,katika kipindi hiki cha uchaguzi oktoba mwaka huu.

Aidha Chama cha waandishi wahabari mkoa kinawashauri waandishi kutojihusha na kuripoti matokeo yoyote ya uchaguzi bila ruhusa ya Tume ya Taifa ya uchaguzi au mamlaka zinatabuliwa na Tume. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii