Tamasha la Land Rover Iringa 2025 litakalofanyika mwezi Novemba 2025 linatarajia kutangaza vivutio vya utalii vya mkoa wa Iringa hivyo kuvutia watalii wengi kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mahojiano maalum Mjumbe wa Kamati ya Uratibu la Land Rover Bw. Augustine Namfua amesema mojawapo ya program ya Tamasha hilo ni kufanya camping katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
« Mpaka sasa tumepokea usajili wa wageni kutoka nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi na Zambia ambapo tunatarajia kuwa na Land Rover zaidi ya 200 » amesema Bw. Namfua.
Aidha amesema kutangazwa kwa filamu ya Tanzania the Royal Tour kumeongeza hamasa kwa washiriki kutoka nchi za nje.
Amesema pamoja na Utalii Tamasha hilo pia litatumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji kwa kutembelea vituo vya watu wenye mahitaji maalum.
Tamasha hilo litakalofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Novemba 2025 Iitaanzia viwanja vya Kihesa Kilolo kuzunguka mjini mpaka viwanja vya Samora.