WANAOHAMASISHA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Filemon Makungu amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwafichua wahalifu wanaohamasisha uvunjifu wa amani na usalama ndani ya jamii ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Hayo yamesemwa Oktoba 16 mwaka huu wakati akitoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Wananchi kulinda na kuimarisha amani,utulivu na usalama kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi kupitia redio Joy Fm ambapo amesema ni jukumu la kila mwananchi kulinda amani,utulivu na usalama uliopo kwa kuwaripoti wahalifu wanaohamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani ndani ya jamii.

SACP Makungu amewataka waendesha Wananchi hao kutii sheria na kutojihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Pamoja na hayo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kubaini,kuzui na kutanzua uhalifu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii