Jera miaka 30 kwa kosa la ubakaji

Mahakama ya Wilaya ya Kasulu imemhukumu mshitakiwa Serikali Machene Lubatula ( 25),mkulima, mkazi Kigembe wilayani Kasulu kifungo cha kwenda jela miaka 30 baada ya kumtia hatia kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 11.

Mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 6 mwaka huu huko Kijiji cha Kigembe wilayani Kasulu na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari mwaka huu.

Akitoa hukumu hiyo Oktoba 13 mwaka huu Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Sara Mcharo amesema kuwa Mahaka imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria,maadili na ukatili dhidi ya watoto.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii