Hayo yameelezwa na mtaalam mkuu wa usalama mtandaoni Yusuph Kileo alipokuwa akizungumza na Jembe fm ambapo alipokuwa akitoa elimu ya usalama mtandaoni ikiwa dunia inaadhimisha siku ya usalama mtandaon ifikapo oktobar kila mwaka
Amesema ni kosa
kisheria kusambaza taarifa ghushi mitandaoni na badala yake watumie mitandao
kwa kujinufaisha katika mambo mbalimbali ambayo yatawaletea faida na hata
kipato.
Nae Hafidhi Masoud mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
kitengo cha ulinzi na usalama wa Tehama Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Amewasisitiza wananchi kuwa na utaratibu wa kubadili Nywila kila baada
ya siku 72 na Nywila hizo zinatakiwa kuwa madhubuti ili kuepusha kudukuliwa kwa
taarifa binafsi na wametakiwa kutoa taarifa pindi watakapoona ujumbe wenye viashiria vya utapeli wa kimtandao kupitia namba 15040.