Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam leo itaendelea na usikilizaji wa maombi ya dharura namba 24511 ya mwaka 2025 yaliyofunguliwa na Humphrey Polepole dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake wanne (4) ambapo maombi hayo yaliyofunguliwa kupitia Wakili Peter Kibatala, yanasikilizwa mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Salma Maghimbi.
Tayari Mama wa Humphrey Polepole Anna Marry amefika Mahakamani hapo kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo leo ambapo sehemu ya maombi hayo ni kwamba Wakili Kibatala anaiomba Mahakama kutoa amri ya haraka ili wajibu maombi wamlete Mahakamani mleta maombi (Humphrey Polepole) leo hii wakati wanasubiri kusikiliza hoja za pande zote mbili (2).