Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokuwa inaendelea katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeahirishwa hadi kesho Oktoba 16 mwaka huu.
Kesi hiyo ilikuwa ikiendelea leo kwa shahidi wa pili kuendelea kuulizwa maswali lakini hata hivyo, Upande wa Jamhuri uliomba ahirisho ili waweze kushiriki maziko ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Asha Hamis Mwetindwa.