Rais William Ruto ametangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa muda wa siku saba kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Amollo Odinga.
Ambapo katika kipindi hicho bendera zote za taifa zitapeperushwa nusu mlingoti kama ishara ya heshima na maombolezo.
Aidha Rais Ruto ametangaza kusitisha shughuli zake zote za umma na kuwasihi maafisa wengine wa serikali kuchukua hatua kama hiyo ili kutoa nafasi ya kutafakari na kuomboleza maisha ya kiongozi huyo mashuhuri.
Hivyo maandalizi ya mazishi ya kitaifa Rais Ruto ametangaza kuundwa kwa kamati maalum ya kushughulikia shughuli hizo itakayokuwa chini ya uongozi wa Naibu Rais Kithure Kindiki.
Wakati huo huo ujumbe wa viongozi wakuu wa serikali ukiongozwa na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi uneondoka nchini Kenya kuelekea India haraka iwezekanavyo ili kushughulikia mipango ya mwisho ya usafirishaji wa mwili wa marehemu.
Hata hivyo rais Ruto amemsifu Raila Odinga kama mtu asiye na tamaa ya makuu, mpenda amani na mzalendo wa kweli, huku Serikali ya India kwa ushirikiano wa karibu na serikali ya Kenya meahidi kugharamia na kuratibu shughuli za kusafirisha mwili wa marehemu kutoka India hadi Kenya kwa ajili ya mazishi