Meya wa Odesa avuliwa uraia na Zelensky

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemvua uraia Meya wa Odesa, Gennadiy Trukhanov, kwa madai ya kumiliki pasi ya kusafiria ya Urusi. Hatua hiyo imezua mtafaruku wa kisiasa katika jiji hilo muhimu la bandari ambalo limekuwa ngome ya kiuchumi na kijeshi katika vita inayoendelea na Urusi.

Idara ya Usalama ya Taifa (SBU) ilitangaza kupitia Telegram kwamba amri hiyo imesainiwa na Rais Zelensky, ikimtuhumu Trukhanov "kuwa na uraia wa nchi mshambuliaji.” Kwa mujibu wa katiba ya Ukraine, raia mwenye uraia wa nchi adui hapaswi kushikilia nafasi ya umma.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii