Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Isdory Mpango, amewasili katika Viwanja vya Sokoine jijini Mbeya kushiriki kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025.
Katika hatua hiyo Hafla hiyo pia imeambatana na kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14 ,1999.
Aidha Mhe Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo atazungumza na wananchi na kuongoza shughuli mbalimbali za kitaifa zinazoambatana na maadhimisho hayo muhimu.
Hata hivyo Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, wanafunzi pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini.