MANISPAA YA GEITA YANG’ARA KITAIFA KATIKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeibuka mshindi wa kwanza kitaifa katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ikiongoza miongoni mwa Halmashauri zote nchini. Ushindi huu ni ushahidi wa mshikamano, ushirikiano na juhudi za pamoja kati ya viongozi na wananchi wa Manispaa.

Kwa moyo wa shukrani, Halmashauri ya Manispaa ya Geita inatoa pongezi na shukurani za dhati kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita inayoongozwa na Mhe. Hashim Komba kwa usimamizi na mwongozo madhubuti uliowezesha mafanikio haya makubwa. Pia, inawashukuru wananchi wote kwa kujitokeza kwa wingi, kushiriki na kuiunga mkono Halmashauri yao katika hatua zote za maandalizi na mapokezi ya Mwenge.

Kilele cha mbio hizo kimehitimishwa leo mkoani Mbeya, ambapo Manispaa ya Geita imetajwa rasmi kuwa mshindi wa kwanza kitaifa. Huu ni ushindi wa heshima na historia kwa Geita, unaothibitisha dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo ya watu kupitia miradi yenye tija.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii