Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Oktoba 13 mwaka huu amekagua Maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Baba wa Taifa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika ukaguzi huo Waziri Mkuu Majaliwa aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratiba, Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe. Hamza Juma na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa .
Akizungumza mara baada ya ukaguzi Waziri Mkuu alisema ameridhika na taarifa iliyotolewa na Waziri Kikwete kuhusu maandalizi ya miundombinu, hamasa, mapokezi ya wageni na masuala mengine muhimu kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofikia tamati leo Oktoba 14 mwaka huu jijini Mbeya
.