Majaliwa ashiriki ibada ya kumwombea baba wa taifa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Oktoba 14 mwaka huu ameshiriki katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi Mwanjelwa Mkoani Mbeya. 

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango pia ameshiriki katika ibada hiyo.

Ibada hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii