Wanajeshi wachukuwa madaraka baada ya rais kuondolewa na Bunge

Bunge la taifa la Madagascar limepiga kura ya kumuondoa Rais Andry Rajoelina kwa kura nyingi (130 kati ya wabunge 163) siku ya Jumanne, Oktoba 14. Katika taarifa iliyotolewa muda mchache baadaye, Mahakama Kuu ya Kikatiba imemtaka Kanali Michael Randrianirina kushika madaraka ya mkuu wa nchi. Rais wa Madagascar, kwa upande wake, ameshutumu "jaribio la mapinduzi ya kijeshi."

Hali hiyo inajirudia Madagascar: jeshi limedai siku ya Jumanne "kuchukuwa mamlaka," na kumaliza vyema utawala wa Andry Rajoelina, ambaye aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2009 chini ya mazingira kama hayo.

Kikosi cha kijeshi kilichojiunga na vuguvugu kubwa la waandamanaji kwenye kisiwa hiki maskini cha Bahari ya Hindi kilitoa tamko hili mbele ya ikulu ya rais katikati mwa mji wa Antananarivo, mara tu baada ya kura iliyopigwa na Bunge kumtimua mkuu wa nchi, ambaye anashukiwa kuwa ameondoka nchini.

"Tutachukua mamlaka leo na kuvunja Seneti na Mahakama Kuu ya Kikatiba. Tutaacha Bunge la taifa liendelee kufanya kazi," Kanali Michael Randrianirina amekiambia kituo cha televicheni cha AFPTV nje ya ikulu ya rais katikati mwa mji mkuu wa Madagascar.

Matukio ya sherehe na matamasha yalitangulia tangazo hili kwenye eneo la Mei 13. Bendera za Madagascar na nyimbo za sherehe zilijaa mahali hapa pa ishara, palipopewa jina la heshima kwa wale waliouawa wakati wa uasi wa 1972 ambao ulisababisha kuondolewa kwa rais wa kwanza.

Mahakama Kuu ya Kikatiba, baada ya kutambua "nafasi" ya ofisi ya rais, "inaitaka" katika taarifa "mamlaka ya kijeshi yenye uwezo, iliyojumuishwa na Kanali Randrianirina Michaƫl, kutekeleza majukumu ya Mkuu wa Nchi."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii