Kijana mmoja raia wa Uingereza amejikuta akitupwa Jela kwa kosa utapeli kupitia mahusiano ya kimapenzi ili kujipatia kiasi kikubwa cha Pesa kwa ajili ya Kamali.
Kwa mujibu wa Mtandao wa “Daily Mail Uk”, Ben Millin (32) ametapeli jumla ya Paundi 40,000 (sawa na Tshs. 140,384,120/=) kutoka kwa Wanawake Wanne tofauti ambao amekuwa nao katika mahusiano kwa nyakati tofauti akitumia visingizio mbali mbali ikiwemo kufiwa na dugu zake, akaunti zake za bank kufilisika, usaili wa Kazi, na matatizo makubwa ya kiafya.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa wanawake hao ambao wamelalamika sana kuhusu kuvunjiwa haki zao za msingi katika uaminifu wa kimapenzi na Bw. Milin ambaye ni mkazi wa mji wa Yeovil uliopo nchini humo, baadhi yao walifikia hatua mpaka kuuza mali zao za urithi ili kumsaidia mtuhumiwa katika hatua zake hizo za kitapeli
Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina la Fiona aliongeza kuwa, Miling alimpa taarifa kuwa amenyang’anywa mali zake zote na “Ex” wake, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa ajili ya mahitaji na safari ambazo alitakiwa azifanikishe kwa ajili ya majukumu yake.
Wakati Fiona akiendelea na mahusiano na Muhumiwa, haikupita muda Kijana huyo akakamatwa kwa kosa la kumtapeli mwanamke mwingine, ambapo baada ya kuachiwa, alianza utaratibu wa kumtapeli mwanamke mwingine tena aliyeitwa Charlotte, na kisha kuhamia kwa mwanamke mwingine ,Sophie ambaye alikuwa ni mwenye nyumba wake , lakini mahaba yalinoga na kuanza kuishi naye pamoja