Maelezo ya mashahidi wa Lissu kusomwa August 18

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anatarajiwa kusomewa maelezo ya mashahidi Agosti 18 mwaka huu katika kesi  ya uhaini inayomkabili ndani ya  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hatua hiyo inakuja baada ya mvutano wa kisheria baina ya Lissu anayejitetea mwenyewe dhidi ya Jopo la Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franko Kiswaga anayesikiliza shauri hilo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Kiswaga alisema: 

“Mawasilisho ya pande zote mbili, yatanifanya niahirishe kesi hii kwa sababu ya kuandaa maamuzi, kwahiyo leo hii nitaahirisha hadi tarehe ijayo kwa ajili ya kufanya commital procedure na sio tarehe tena kwa ajili ya maamuzi haya mawasilisho nitayatolea amri kwa tarehe hiyo kwa kuzingatia maamuzi ya Mahakama Kuu ambayo yalikuwa wazi yanahusu sio mashahidi wote bali yanahusu mashahidi ambao ni raia, hii taarifa ni kubwa kweli kweli kwahiyo lazima tujipe muda, 

Tukianza kwenda kwenye mawasilisho tuyatolee maamuzi tutapoteza muda kwahiyo kikubwa hapa nitatolea amri juu ya maombi yaliyoletwa na Upande wa Mashtaka pamoja na mapingamizi ya Upande wa Utetezi”.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii