Kura za maoni kupigwa upya jimbo la Kongwa

Mchakato wa kura za maoni katika Jimbo la Kongwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) unatarajiwa kufanyika upya Agosti 17 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyeongoza kura za maoni, hayati Job Ndugai.

Akitangaza utaratibu mzima, Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala amesema mchakato wa kuchukua fomu utafanyika kwa siku moja ambayo ni Agosti 12 mwaka huu Mkaugala amesema na kura zitapigwa leo kwa utaratibu wa wajumbe ngazi ya kata kama ilivyofanyika Agosti 4 mwaka huu na baadaye vikao vya kawaida vitaendelea.

Mkagula amesema gharama za fomu ni kama ilivyokuwa awali, watalipia Sh500,000 na si vinginevyo. Hata hivyo, hakuweka wazi kama kutakuwa na kampeni za kuzunguka kwa wajumbe kwa ajili ya kuwanadi wagombea kama awali akisema wanachama wasubiri wataelezwa utaratibu.

Katika matokeo ya awali, Ndugai aliongoza kwa kupata kura 5,692, akifuatiwa na Isaya Mngurumi (2,602), Deus Seif (1,260), Dk Samora Mshang’a (544), Dk Simon Ngatunga (517), Elias Mdao (435), Philip Chiwanga (558), Paschal Mahinyila (331), Balozi Emmanuel Mbennah (232) na Ngaya Mazanda aliyepata kura 195.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii