Mgombea Urais wa Tanzania kupitia tiketi cha Tanzania Labour Party (TLP), Yustas Mbatina akiwa ameambatana na Mgombea mwenza wake Amana Mzee, amechukua fomu ya Urais katika Tume Huru ya Uchaguzi Jijini Dodoma August 11 mwaka huu huku akiahidi kuleta matibabu bure kwa wote na kuhakikisha kuwa hakuna Mtu analipia kutoa maiti Hospitali kisa madeni na pia amewaahidi Vijana kuwa wote watakuwa na ajira.
Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu, Mbatina amessma “Vipaumbele vyangu ni ulinzi na usalama wa nchi, utawala bora na uchumi imara, nitaimarisha uchumi, tuna Vijana wengi wamemaliza Shule hawana kazi, lazima Vijana tuhakikishe uchumi imara ili tuwatafutie Vijana kazi ya kufanya”
“Tuna tatizo la afya ni lazima afya iimarike zaidi , Mahospitali yapo lakini hayana madawa na Watu hawana hela za kununua madawa, Mtu anafikiri unadaiwa hela ukalipie maiti na hela huna , maiti nyingi zinazikwa na City Watu wanazizira hilo sisi tunasema matibabu ni bure na tutaimarisha mifuko ya bima hata Bodaboda, mfugaji, mzoa taka barabarani watakuwa na bima, sisi tunasema elimu bure, matibabu bure tutazunguka nchi nzima mtupe nchi tutekeleze tuliyoyaahidi”