CCM kesho kufanya mkutano wa kuchangia pesa za wagombea Urais kupitia Chama hicho

Chama cha Mapinduzi CCM kimetoa wito kwa Wanachama na Wafuasi wa Chama hicho kujitokeza kesho August 12, katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya Harambee ya kutafuta Mchango wa Udhamini kwa Wagombea wa Urais kupitia Chama hicho.

Haya yamebainishwa leo August 11, Jijini Dar es salaam na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi Mgombea Mwenza Wa Urais Kupitia CCM, na kwamba Chama hicho kinakusudia kukusanya mchango wa Shilingi Bilioni 100, akiongeza kuwa hata vyama vingine vinaruhusiwa kuchangia katika mchango huo.

Dkt. Nchimbi ameweka bayana kuwa Mgeni Rasmi katika Harambee hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hatua hii inakuja baada ya Juzi August 9, Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na Mgombea mwenza, Wafuasi na Wanachama kuchukua Fomu katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii