Luhaga Mpina asisitiza umuhimu wa Muungano

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema wananchi wa Zanzibar wanataka mamlaka kamili, akisisitiza kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliwekwa na Watanzania wenyewe na maamuzi yake pia yanapaswa kufanywa na Watanzania.

‎‎Akihutubia mkutano wa hadhara kisiwani Pemba, Mpina alisema hakuna sababu ya mtu yeyote kupinga maoni ya wananchi kuhusu mustakabali wa Muungano, na kwamba anayefanya hivyo hawezi kudai anasimamia maslahi ya umma bali anatafuta maslahi binafsi.

‎‎Ameeleza kuwa wananchi wengi wanapendelea mfumo wa Serikali tatu, na akauliza wazi: “Kuna tatizo gani kuwa na Serikali tatu?” Mpina alisema changamoto nyingi zinazotajwa kuwa za Muungano zimekuwepo kwa muda mrefu, hivyo ni muhimu kutafuta suluhisho la kudumu badala ya kuendelea kuzieleza bila kuzitatua.

‎‎Amesema tatizo kubwa ni kukosekana kwa viongozi wenye ujasiri wa kuchukua hatua, na kwamba ACT-Wazalendo imekuja na kizazi kipya cha viongozi vijana waliyo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko chanya na kulinda maslahi ya Watanzania wote.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii