Aiburuza Mahakamani Kampuni yake Kwa Kumlipa Mshara Miaka 20 Bila Kufanya Kazi

Mwanamke mmoja raia wa Ufaransa amefungua mashtaka dhidi ya kampuni anayoifanyia kazi, kwa kumlipa mshahara kwa miaka 20 bila kupewa majukumu yoyote ya kikazi

Bi. Laurence Van Wassenhove (56) amesema kuwa ameamua kufungua mashtaka hayo kutokana na muajiri wake kumfanya asionekane muhimu katika kampuni hiyo kwa kutokumpangia majukumu yoyote yale huku akiendelea kupokea mshahara wake kama kawaida, jambo ambalo limekuwa likimuathiri kisaikolojia kwa muda mrefu sasa

Katika mashitaka yake , Bi. Laurence anasema kuwa, hiyo ni tafsiri tosha ya ubaguzi mkubwa kwake unaofanywa na kampuni ya simu nchini humo inayofahamika kwa jina la ORANGE kwa kumfanya asionekane katika majukumu yake ya kila siku, na kumnyima haki yake ya kujumuika na wafanyakazi wenzake kwa ajili ya kushirikiana katika majukumu yao ya kila siku na kumfanya awe “Mtumishi Hewa”

Aidha mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto wawili anadai kuwa, alikuwa ni mtu mwenye furaha alipotaarifiwa kuwa amepata kazi katika kampuni hiyo kubwa ya simu nchini Ufaransa mnamo mwaka 1993, lakini hali ya unyanyapaa ilianza kuonekana baada ya kupata tatizo matatizo ya kiafya yaliyopelekea kupooza upande mmoja, na kumfanya asifanye kazi tena kwa ufanisi

Laurence ni mbobezi katika idara ya Rasilimali Watu (Human Resource), aliajiriwa na kampuni hiyo akiwa kama Afisa Rasilimali Watu Msaidizi (Assistant HR), na hivi sasa bado anaendelea kupokea Mshahara ambao haufanyii kazi yoyote kwa takribani miaka 20.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii