J Lo Agoma Kuingia Dukani Baada Ya Mlinzi Kushindwa Kumtambua

Msanii wa Muziki wa Pop na R&B nchini Marekani Jennifer Lopez maarufu kama “J-Lo”, aligoma kuingia katika duka la fashion la CHANEL liliko Istanbul,Uturuki baada ya Mlinzi kushindwa kumtambua,

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa “Turkey Today”, “Bibie” huyo ambaye pia ni Muigizaji wa Filamu nchini Marekani, alifika katika Duka hilo “la kishua” kwa ajili ya kufanya mahemezi ya bidhaa mbali mbali ambazo alizihitaji, lakini ghafla mlinzi alimzuia kuingia na kumwambia kuwa ndani ya duka palikuwa pamejaa watu wengi, hivyo hawezi kuruhusu mtu mwingine aingie ndani.

Jibu la J Lo kwa mlinzi huyo lilikuwa ni “Sawa, hakuna shida” na kisha akaondoka na kuelekea katika duka liliokuwa limepakana na Duka la Chanel kisha kuanza “kumwaga” pesa za kutosha kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa alizokuwa anahitaji

Hata hivyo, baada ya wasimamizi wa duka hilo kubaini kuwa aliyezuiwa kuingia alikuwa ni mtu maarufu sana na muhimu haswa, walijitahidi kumuhimiza na kumsihi arudi kwa ajili ya manunuzi yake kwa sababu Mlinzi hakumtambua, J Lo (56) alikataa “katakata” huku akielekea katika duka la Celine &Beymen ambako alifanya mahemezi yake kwa takriban masaa matatu kabla ya kuondoka

 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii