Watiwa hatiani kwa uhalifu kura za maoni

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kujihusisha na jaribio la kufanya uhalifu wakati wa zoezi la uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) jimbo la Vunjo.

Watu hao wanadaiwa usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura za maoni, yaani Agosti 4,2025 walionekana wakiwa na silaha za jadi,mabomu pamoja na kamba ngumu na walimjeruhi kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Safina ambaye taarifa za kushambuliwa kwake aliripoti katika kituo cha Polisi Himo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alipoulizwa juu ya suala hilo alisema atafutwe aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni katibu wa chama hicho ngazi ya mkoa.

Aidha taarifa kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro zinaeleza kuwa gege hilo liliratibiwa kwa karibu zaidi na mmoja ya waliokuwa wanania kupata nafasi ya kuwakilisha jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu, baada ya mmoja wa watuhumiwa wa genge hilo la uhalifu aliyekamatwa na Polisi kuwa na uhusiano  naye wa kindugu.

Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa ni kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini wote walionyuma ya kundi hilo la kihalifu ikiwemo taarifa za zinazomhusisha mmoja wa waliokuwa wagombea wa nafasi ya ubunge kwenye kura za maoni CCM Vunjo kuhusika na kundi hilo lililopanga kuvuruga uchaguzi huo.

Uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro

ulikuwa na jumla ya wagombea sita ambapo matokeo ya uchaguzi huo, Enock Koola aliibuka mshindi kwa kupata kura (1999), Dkt Charles Kimei (861), Yuvenal Shirima (659), Didas Lyamuya (329),Prosper Tesha (177) na Delfina Kessy aliambulia kura (29).

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii