Job Ndugai kuzikwa leo katika Kitongoji cha Mandumbwa

Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Hayati Job Ndugai ambaye alifariki dunia August 06 mwaka huu anazikwa leo August 11,2025 shambani kwake katika Kitongoji cha Mandumbwa kilichopo Kijijj na Kata ya Sejeli Wilayani Kongwa Mkoani 

Vyombo mbalimbali vya habari vimefika katika eneo hilo na kuongea na Watu mbalimbali akiwemo Mdogo wake Ndugai aitwaye Bahati Edward ambaye amesimulia jinsi alivyokutana na Ndugai siku mbili kabla ya kifo chake na jinsi alivyosimamia kura za Ndugai kwenye mchakato wa kura za maoni katika kituo cha Songambele hadi Ndugai alipotangazwa Mshindi na akamuandikia Ndugai ujumbe wa kumpa matokeo na pongezi August 04 mwaka huu saa tatu usiku ambapo Ndugai alimjibu.

Bahati pia ametuonesha gari la kwanza ambalo Ndugai alilitumia wakati wa kampeni zake mwaka 2000 na ambalo alilipenda sana na akaamua kulihamishia shambani kwake ili kumbukumbu isipotee.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii