Michuano ya CHAN yazidi kupamba moto katika nchi tatu za Afrika mashariki

Michuano ya CHAN2024 inaendelea katika nchi tatu wenyeji Kenya, Tanzania na Uganda, ambapo hii leo mechi kadhaa zitasakatwa katika kundi C nchini Uganda.

Katika kundi C, mwendo wa saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki, Afrika Kusini watavaana na timu ya Guinea katika uwanja wa Mandela nchini Uganda, kisha baadaye saa mbili usiku Uganda watakutana na Niger katika uwanja huo huo.

Tukiangazia mechi za hapo jana, nchini Kenya, timu ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wake na kuibuka na ushindi wa bao moja bila dhidi ya mabingwa mara mbili Morocco katika kundi Bao la ushindi lilifungwa na Ryan Ogam katika dakika ya 42 na sasa Kenya inashikilia nafasi ya kwanza kwenye kundi A baada ya kucheza mechi tatu ikiwa imejizolea alama saba.

Baadaye jioni ilikuwa zamu ya Zambia na Angola, ambapo Kaporal aliyetoka kwenye benchi alifunga mabao mawili katika dakika 11 za mwisho huku Zambia ikijibu kwa moja, ushindi wa Angola ukuzima matumaini ya Zambia ambayo baada ya mechi tatu haina alama yoyote.A, licha ya Crispine Erambo kuonyeshwa kadi nyekundu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii