David Bekham Aingiwa Na Hofu. Ni Kuhusu Mtoto Wake Mkubwa

Mwanasoka mstaafu wa Timu ya Taifa ya Uingereza, David Bekham pamoja na mke wake Victoria Bekham, wameingiwa na hofu juu ya mtoto wao mkubwa Brooklyn Bekham kujiweka mbali na familia hiyo, baada ya kutomshirikisha ndugu yeyote katika hafla ya kutia nadhiri ya ndoa yake  kwa mara ya pili.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Familia hiyo, Brooklyn na mke wake Nicole Peltz walifunga ndoa rasmi mwaka 2022 ambayo ilihudhuriwa na ndugu wote ikiwemo wazazi wake na wadogo zake, lakini cha ajabu ni kwamba, wakati wakitia nadhiri kwa mara ya pili (Vow Renewal) ili kuimarisha ndoa yao na kusherekea mafanikio ya ndoa hiyo, hakuna mwanafamilia yeyote wa David Bekham aliyepewa taarifa wala mwaliko, kitu ambacho kimewapa hofu Zaidi ya mtoto wao kujitenga na familia hiyo.

Aidha, taarifa zinaeleza kuwa, shughuli hiyo ambayo ilifanyika katika Jimbo la Westchester lililopo New York nchini Marekani, Agosti 2, 2025 lilihudhuriwa na marafiki pamoja wazazi wa upande wa mke wake Nicole, huku Familia ya Bekham ikipata taarifa kupitia tovuti ya The Sun iliyoshuhudiwa na wadogo zake kisha kuwaataarifu wazazi wao.

Tukio hilo lilionekana kumvunja moyo David Bekham ambaye amewahi kukipiga katika Vilabu vya Manchester United na Real Madrid, kwani hakuona sababu ya kijana wao huyo kutokuishirikisha familia yake katika tukio muhimu kama hilo.

Hata hivyo, dalili za Broklyn kujiweka mbali na familia yake zilianza kuonekana mapema baada ya kupuuzia Sherehe ya David Bekham (Baba yake) alipokuwa akiadhimisha miaka 50 ya Kuzaliwa kwake


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii