Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuchangisha jumla ya shilingi Bilioni 86.31 katika harambee ya kuchangia kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 katika tukio hilo liliofanyika usiku wa Agosti 12 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.
Harambee hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan, Wafanyabiashara, Wadau wa maendeleo pamoja na Wageni mbalimbali waalikwa.
Michango hiyo ni sehemu ya malengo ya CCM ya kukusanya Shilingi Bilioni 100 ambapo Uongozi wa Chama umeeleza kufurahishwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa Wanachama na Wafau na kusisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema kwa ushindi wa Chama hicho.