DARFUR, SUDAN : SHIRIKA la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeripoti kuwa takriban watu 40 wamefariki dunia katika eneo la Darfur, Sudan, kufuatia mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa kipindupindu.
Kwa mujibu wa MSF, Darfur ni eneo kubwa la magharibi ambalo limekuwa kitovu cha mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) kwa zaidi ya miaka miwili ndilo ambalo limeathirika zaidi na mlipuko huo uliodumu kwa mwaka mzima.
Taarifa ya shirika hilo imeeleza kuwa katika wiki moja iliyopita pekee, madaktari walioko Darfur walipokea wagonjwa zaidi ya 2,300 na kuripoti vifo 40. yohusishwa na kipindupindu vimeripotiwa kati ya wagonjwa 99,700. MSF imesema uhamishaji mkubwa wa raia kutokana na vita umechochea mlipuko huo kwa kuwanyima watu maji safi ya kunywa na kwa matumizi ya usafi wa msingi, kama kuosha vyombo na chakula.
Kwa sasa kiasi cha maji kinachopatikana ni wastani wa lita tatu kwa mtu kwa siku ambayo ni chini ya nusu ya kiwango cha dharura cha lita 7.5 kinachohitajika kwa kunywa, kupika na usafi wa mwili.