Klabu ya Yanga imeanza rasmi mchakato wa kuwarahisishia wawekezaji na wabia wa kimkakati kuwasilisha barua za kuonesha nia (EOI) kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa eneo la Jangwani/Twiga Street, jijini Dar es Salaam.
Uwanja huo unaopangwa kujengwa utakuwa na uwezo wa watazamaji 25,000–35,000, ukiwa na hybrid pitch, maeneo ya VIP, mifumo ya kisasa ya usalama, taa za jioni, umwagiliaji wa kisasa, pamoja na miundombinu ya kibiashara inayolenga kuongeza mapato ya klabu.
Yanga SC imeonyesha kuwa iko tayari kuingia katika ubia kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na Naming Rights, Sponsorship-led Funding, PPP (Public-Private Partnership) na DBFO (Design, Build, Finance, Operate), kama sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuimarisha mapato na maendeleo ya klabu.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha EOI ni Januari 23, 2026 saa 10:00 jioni.
Hatua hii ni ishara wazi ya dhamira ya Yanga SC ya kujenga uwanja wa viwango vya kimataifa, huku ikilenga kuendelea kuimarisha hadhi ya klabu kitaifa na kimataifa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime