Hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kisa mafuriko

Wananchi hao wameiomba serikali kurejesha huduma muhimu kama umeme maji pamoja na kutuma wataalamu kuja kutibu madimbwi ya maji yanayozagaa mtaani ili waweze kuepukana na magonjwa ya mlipuko. 

Wananchi wa kijiji cha Ntinga kata ya Msangano wilayani Momba mkoani Songwe wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na maji yaliyotapakaa mtaani kutokana na mafuriko yaliyotokea siku ya jana January 8 na kusomba vyoo pamoja na kuharibu miundombinu ya visima vya maji wanayotumia.

Hali ya kawaida imerejea kama kawaida katika kijiji hicho lakini wananchi wameiomba serikali kurejesha huduma muhimu kama umeme maji pamoja na kutuma wataalamu kuja kutibu madimbwi ya maji yanayozagaa mtaani ili waweze kuepukana na magonjwa ya mlipuko. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii