Watu 6 Wafariki Maporomoko ya Mgodi wa Koltani Rubaya

Watu wasiopungua sita wamepoteza maisha Jumanne baada ya shimo kuporomoka katika mgodi wa koltani uliopo Rubaya, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hata hivyo, ripoti nyingine zinaeleza kuwa huenda hadi watu 100 wameangamia katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa mashahidi waliolizungumza na shirika la habari la AFP, wanaume watatu na wanawake watatu walifariki katika mgodi huo ulioko takriban kilometa 70 magharibi mwa mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Machimbo ya koltani ya Rubaya yanadhibitiwa na waasi wa M23, ambapo maelfu ya wachimbaji wadogo hufanya kazi katika mazingira hatarishi wakitumia zana duni kama chepeo na sururu.

Aidha  kasa ni wa pili katika maporomoko ya udongo kuripotiwa katika eneo hilo ndani ya wiki za karibuni ambapo serikali inakadiria kuwa watu wapatao 200 walipoteza maisha katika tukio kama hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi uliopita.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii