Hatua hiyo imekuja kufuatia ukaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kitengo cha usalama barabarani mkoani humo kubaini kuwa kati ya magari 20 yaliyokaguliwa,matano yamekutwa yakiwa mabovu.
Wito umetolewa kwa madereva wa magari yanayotumika kubeba wanafunzi wa shule kabla ya siku chache zijazo kwa shule kufunguliwa, kuhakikisha kuwa magari mabovu hayatumiki ili kuhakikisha usalama wao.
Hatua hiyo imekuja kufuatia ukaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kitengo cha usalama barabarani mkoani humo.
Akiwa katika ukaguzi huo Mkuu wa Kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Katavi Leopord Fungu amesema katika ukaguzi huo jumla ya magari 20 yamekaguliwa, kati ya hayo matano yamekutwa yakiwa mabovu na kuagiza yafanyiwe marekebisho kabla ya kuanza kazi ya kubeba wanafunzi pindi shule zitakapo funguliwa mapema wiki ijayo.
Nao baadhi ya wazazi na walezi wamesema hatua ya kufanyika kwa ukaguzi huo wa magari itasaidia kuleta tahadhari ya usalama kwa wanafunzi pindi shule zitakapofunguliwa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime